Skip to main content

Dunia yaadhimisha siku ya Mandela

Dunia yaadhimisha siku ya Mandela

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema siku hii ni fursa ya kukumbuka maisha na kazi ya mtu aliyepigania amani, hadhi ya mwanadamu, na dunia bora.

Jijini New York Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku hii kwa matukio mbalimbali ikiwamo kazi za kujitolea kusaidia wahitaji, huku pia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiwa na tukio la kumuenzi shujaa huyo.

Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na ubalozi wa Afrika Kusini umeadhimisha siku hiyo kwa kuwatembela na kuwafariji wagonjwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

Dk Julius Mwaisege ni Mkurugenzi Mtendaji wa tasisi ya saratani ya Ocean Road.

(SAUTI DK JULIUS)