Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mlolongo wa mashambulizi ya kigaidi Lebanon

Ban alaani mlolongo wa mashambulizi ya kigaidi Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mlolongo wa mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga yaliyofanyika jana na kwenye mji wa El-Qaa Kaskazini Mashariki , kwenye mpaka na Syria.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo na majeruhi wengi. Ban ametuma salamau za rambirambi kwa familia za wahanga wa vitendo hivi vya kigaidi , na pia kwa serikali ya Lebanon , huku akiwatakia afueni ya haraka majeruhi.

Ban amesema Umoja wa Mataifa unashikamana na Lenabon katika kukabili vitisho vya ugaidi na changamoto zingine za kiusalama.

Pia amepongeza jukumu kubwa linalofanywa na vikosi vya jeshi la Lenbanon na kuvichagiza kuendelea na juhudi za kulinda ana kuhakikisha utulivu na usalama nchini humo kwa msaada mkubwa wa kimataifa