Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vizuizi vya Israel Ukanda wa Gaza vikome ni adhabu ya jumla:Ban

Vizuizi vya Israel Ukanda wa Gaza vikome ni adhabu ya jumla:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa wito Jumanne wa kumalizika kwa vizuizi vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza , na kuvielezea kama ni adhabu ya jumla. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye shule inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa mjini Gaza Ban amesema vizuizi hivyo vinaongeza madhila , kuathiri mambo mengi na kwamba

(SAUTI YA BAN)

“Wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha na kufungwa kwa Gaza, kunawapa madhila watu wake, kunadumaza uchumi, na kuathiri juhudi za ujenzi mpya. Ni adhabu ya jumla na kwa hivyo kunahitaji kuwe na uwajibikaji”.

Ameongeza kuwa hali hii haiwezi kuendelea , inachagiza chuki na hamasa, inaongeza hatari ya kuzuka kwa uhasama mpya ambao utazidisha adha kwa watu wa Gaza.