Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki- Nadi

Neno la wiki- Nadi

Katika Neno la Wiki hii  Ijumaa Juni 24 tunaangazia neno nadi na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Onni Sigalla anazungumzia maana ya neno nadi na matumizi yake anasema neno nadai lina zaidi ya maana moja. Kwanza ni tanagaza jambo kwa sauti kubwa , amsha watu asubuhi na mapema kwenda kusuali . Pia nadi nyingine yenye mashiko zaidi kwa watu ni ile ya kutangazia wanunuzi bei ya kitu kwa sauti katika mnada, ambapo watu hushindana bei na ndipo mmoja hushinda na kununua. Maana nyingine ni mahali au makazi ya kustarehe hasa wakati wa mazungumzo lakini pia unaweza kupaita mahali hapo klabu.