Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU wafanya ziara kusaka amani Burundi

AU wafanya ziara kusaka amani Burundi

Ujumbe wa  Baraza la Usalama na Amani la Muungano wa Afrika AU uko ziarani nchini Burundi katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa nchini humo. Katika ziara hiyo ya siku mbili ujumbe huo utakuwa na mazungumzo na wadau mbalimbali wa siasa. Kutoka Burundi mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani  Kibuga anaripoti zaidi.

(Taarifa ya Kibuga)

Ujumbe huo wa mabalozi 15 wa Baraza la Usalama na amani la Muungano wa Afrika unaongozwa na Muakilishi wa kudumu wa nchini Congo Brazzaville katika Shirika la AU Bwana Lazare Makayat Saofuesse watakuwa na mazungumzo na wadau mbali wa siasa za burundi kuanzia wakuu serikalini, mashirika ya kiraia, viongozi wa madini lakini pia Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Bwana Lazarre Makayati amesema lengo la ziara yao ni sehemu ya juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Burundi.

(Sauti Makayati)

"Tuko hapa kuleta ujumbe wa matumaini na wa mshikamano kwa ndugu zetu warundi na kujaaribu kutoa msukumo kwa juhudi zote zilizofanywa hadi wakati huu , hivo tumekuja kuwaskiza wadau wote na kuona na jinsi gani tunaweza kufanya ili Burundi irudi kupata amani ya kudumu." 

Ziara ya Baraza la Amani na Usalama la AU ineafuatia ile iliyofanywa na Marais watano wa Muungano wa Afrika mwezi February mwaka huu ambao waliagiza mazungumzo shirikishi ili kumaliza mgogoro wa Burundi.

Awali , wakati wa hali ya ngumu ya mzozo huu, Baraza hilo lilishauri kutumwa walinda amani 5000 ili kujaribu kumaliza ghasio nchini humo. Lakini baadae Mkutano wa Marais wa AU wa mwezi januari waliazimia kuachana na mpango huo baada ya serikali ya Burundi kupinga mpango huo na kutishia kupambana na vikosi hivyo.

Badala yake Muungano wa Afrika uliamua kuwatuma hapa nchini waangalizi 100 wa haki za binaadamu ambao sambamba na waangalizi wa kijeshi waliopo hapa Bdi tangu mwezi septemba mwaka jana.

Burundi imekumbwa na mgogoro wa kisiasa kwa zaidi ya mwaka mmoja kufuatia muhula wa ziada wenye utata wa rais Pierre Nkurunziza. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, watu 500 wameuwawa na raia laki mbili na alfu sabini kutorokea katika nchi jirani.