Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika inahitaji wataalamu wa mipango:UN-Habitat

Afrika inahitaji wataalamu wa mipango:UN-Habitat

Afrika ina upungufu mkubwa wa wataalamu wa mipango waliorodhewa hali ambayo itaathiri vibaya maendeleo ya bara hilo na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-Habitat lina nia ya kushughulikia kasoro hii. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Mkutano baina ya baraza la uandikisaji wataalamu wa miapango miji la Nigeria (TOPREC) na shirika la UN-Habitat umesikia kwamba, Kenya taifa lenye watu zaidi ya milioni 40 lina wataalamu 200 tuu waliorodheshwa.

Hali pia imetajwa kuwa mbaya Nigeria ambayo ina wataalamu wa mipango 400 tuu huku ikiwa na watu zaidi ya milioni 170.

Kwa mujibu wa Rais wa TOPREC Timothy O.Egunjobi kuna uelewa mdogo miongoni mwa waafrika kuhusu jukumu la wataalamu wa mipango, wanaonekana hawana manufaa na kudharaulika.

Lanini amesema kuna matumaini hasa baada ya Kenya kupitisha katiba mpya mwaka 2010 ambayo imewapa wataalamu wa mipango jukumu kubwa katika maendeleo ya jamii.