Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mateso na watu kushikiliwa kinyume cha sheria vyaongezeka Burundi: Zeid

Mateso na watu kushikiliwa kinyume cha sheria vyaongezeka Burundi: Zeid

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa  Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya Jumatatu kwamba kuna ongezeko kubwa la matumizi ya mateso na vitendo vya unyanyasaji nchini Burundi . Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Zeid Pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuwepo kwa mahabusu za kinyume cha sheria mjini Bujumbura na viunga vyake. Amesema tangu mwanzo wa mwaka timu ya haki za binadamu imeorodhesha visa vipya 345 vya utesaji na unyanyasaji.

Ameongeza kuwa takwimu hizi za kushangaza ni ishara ya wazi ya kuenea na kuongezeka kwa vitendo vya utesaji na unyanyasaji vinavyofanywa na vikosi vya usalama vya serikali. Cecile POUILLY  ni msemaji wa ofisi ya haki za anasema wito wao kwa serikali ni

(SAUTI YA CECILE  POUILLY)

 “Wito wetu wa kwanza ni kuiomba serikali ya Burundi kusitisha mara moja vitendo hivyo vya mateso. Pia watu waliofungwa kwa muda unaozidi wakati unaotakiwa waachiliwe huru au wafikishwe mahakamnia. Halafu ni kurejea kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu inaonekana Burundi inaendelea kwenye njia inayotia wasiwasi, na mivutano inaongezeka.”

Ameongeza kuwa  vitendo hivyo utekelezwa wakati watu wanapokamatwa, kuwasili au wakiwa kizuizini hasa katika mahabusu zinazoendeshwa na idara ya upelelezi ya taifa, polisi na pia jeshi.