Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo kabla ya uchaguzi Gambia vyaashiria hofu:Zeid

Vifo kabla ya uchaguzi Gambia vyaashiria hofu:Zeid

Kifo cha kiongozi wa upinzani aliyekuwa kizuizini nchini Gambia lazima kichunguzwe na kuwapa msaada wa tiba kuokoa maisha ya majeruhi waliokuwa wakiandamana kwa amani ambao bado wako kizuizini , amesema Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa yake baada ya kifo cha mjumbe wa chama cha United Democratic (UDP) Solo Sandeng, mmoja wa wanaharakati watatu waliouawa baada ya maandamano ya wili iliyopita Zeid Ra'ad Al Hussein , amesema hali hiyo inasikitisha sana na inaashiria mazingira ya hofu kabla yay a uchaguzi Gambia.

Duru zinasema vikosi vya usalama vilivunja maamndamano ya amani wiki iliyopita na kujeruhi vibaya watu wengi. Kwa mujibu wa Ravina Shamdasani msemaji wa ofisi ya haki za binadamu kuna wasiwasi dhidi ya muandamani ambaye bado yuko kizuizini na anahitaji msaada wa haraka.

(SAUTI YA RAVINA)

"Tuna taarifa kwamba mmoja wa waandamanaji ambaye alikamatwa yuko kwenye koma hana fahamu, hivyo ni muhimu sana wapatiwe msaada wa tiba haraka, na huu ni wajibu wa serikali ya Gambia kuhakikisha kwamba wanapata matibabu”

Ameongeza kuwa kufuatia kifo cha kiongozi huyo wa upinzani kumekuwa na maandamano mapya, na kunahofu jinsi gani serikali itawachukulia hatua wakati huu hali ya haki za binadamu ikizidi kuwa mbaya.