Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa biashara ya utumwa katika muziki wa Amerika ya Kusini

Mchango wa biashara ya utumwa katika muziki wa Amerika ya Kusini

Kila mwaka Machi 25, Umoja wa Mataifa huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Waathirika wa Utumwa na biashara ya utumwa.

Katika Umoja wa Mataifa, siku hii imeleta fursa ya kuelimisha jamii juu ya sababu zake, madhara yake na kuongeza ufahamu wa hatari ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi mamboleo na jinsi ya kupambana nayo. Mwaka huu, moja ya hafla za kumbukumbu iliangazia jinsi biashara ya utumwa ilivyochangia katika muziki wa watu wenye asili ya kiafrika hususan Amerika ya Kusini. Assumpta Massoi anakufahamisha zaidi katika makala hii...