Skip to main content

Kobler ataja mambo muhimu kufanikisha mchakato Libya

Kobler ataja mambo muhimu kufanikisha mchakato Libya

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler ametaja mambo yanayopaswa kufanyika hivi sasa ili kuharakisha mchakato wa kuunda serikali ya Umoja wa kiataifa nchini humo baada ya mazungumzo baina ya viongozi waandamizi wa Baraza la wawakilishi nchini humo.

Kobler amesema akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, kufuatia mkutano huo wa rais wa baraza la wawakilishi nchini Libya na maafisa waandamizi wa baraza hilo, mkutano uliofanyika Cairo, Misri tarehe Nane mwezi huu.

(Sauti ya Kobler)

“Mosi ni Baraza la wawakilishi kuridhia makubaliano ya serikali ya pamoja, kwani baada ya hapo kutakuwepo na uhalali. Namba mbili iwapo hilo litafanyika, hiyo serikali inapaswa iandae mchakato wa makabidhiano. Na makubaliano yanasema kufanyike mara moja makabidhiano ya madaraka kwa amani na kwa utaratibu, nasisitiza neno makabidhiano ya mamlaka kwa amani. Hii ina maana upande wa Tabrouk na serikali ya Tripoli waeleze maafisa wao wa serikali Tripoli kuwa kuna mawaziri wapya wako madarakani na wawapatie maelekezo na siyo sisi.”