Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola yakabiliwa na mlipuko wa homa mbaya ya manjano kuwahi kuzuka katika miaka 30:WHO

Angola yakabiliwa na mlipuko wa homa mbaya ya manjano kuwahi kuzuka katika miaka 30:WHO

Angola inakabiliwa na mlipuko wa homa ya manjano ambayo imeathiri watu Zaidi ya 450 na kukatili maisha ya watu 178, ikiwa ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo kulikumba taifa hilo katika kipindi cha miaka 30.

Mlipuko huo ambao uliripotiwa kwanza mji mkuu Luanda desemba mwaka jana sasa umesambaa katika majimbo 6 kati ya 18 ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa Dr Sergio Yactayo mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko wa WHO, mlipuko kama huu mara nyingi huzuka katika maeneo ya misitu ya kitropiki.

Ameongeza kuwa na mlipuko kuanzia mji mkuu Luanda hali ni ya hatari Zaidi na vigumu kuidhibiti kwa sababu ungonjwa unaweza kusambaa kirahisi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na hali imeshaanza kushuhudiwa.

Homa ya manjano inasababishwa na mbu aliyeathirika ambaye anajulikana kama Aedes aegypti mbu ambaye pia huambukiza virusi vya Zika. Watu ambao wameambukizwa na kuathirika vinbaya wasipotibiwa hufa kati ya siku 10 hadi 14.