Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge vijana walenga kumaliza ufisadi na kuimarisha uwazi

Wabunge vijana walenga kumaliza ufisadi na kuimarisha uwazi

Zaidi ya wabunge vijana 130 kutoka mabunge mbalimbali dunia wameelezea utayari wao wa kuimarisha uwazi na usimamizi wa fedha za umma kama msingi wa kukabiliana na ufisadi baada ya kuhitimisha mkutano wa siku mbili katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Wabunge hao ambao walihudhuria kongamano la tatu la vijana wabunge la Muungano wa wabunge duniani, IPU #youngMPs wamefikia makubaliano hayo ya kuimarisha uchunguzi katika bajeti ya taifa kama moja ya mikakati ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs kufikia mwaka 2030.

Mathalani wameridhia mkataba uitwao Ajenda 2030:Vijana wakiongoza, mtu yeyote asiachwe nyuma, ambako wametaja ufisadi kama moja ya changamoto kubwa katika kutekeleza maendeleo sawa na endelevu.

Hayo ni moja ya masuala ambayo mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Seneta kutoka Kenya Mutula Kilonzo jr wa kaunti ya Makueni amemdokezea Grace Kaneiya wa Idhaa hii katika mahojiano maalum, ambapo hapa anaanza kwa kueleza mijadala waliyogusia