Vijana wakipatiwa fursa wanaleta mabadiliko kwenye nchi zao

Vijana wakipatiwa fursa wanaleta mabadiliko kwenye nchi zao

Ushiriki wa vijana katika mikutano ya kimataifa ambako serikali zao zinatoa ahadi, ni muhimu ili kuwezesha ahadi hizo kufuatiliwa na kutekelezwa.

Hiyo ni kwa mujibu wa Aude Isimbi, Mratibu wa shirikisho la vijana wakristo duniani, alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW60 jijini New York, Marekani.

Aude amesema ni kwa mantiki hiyo shirika lao limedhamini mwanafunzi wa kike kutoka Nigeria kuweza kufuatilia kile ambacho serikali yao inasema kwa kuwa..

(Sauti ya Aude)

Amesema hatua hiyo imeleta mabadiliko kwa sababu..

(Sauti ya Aude)

Mkutano wa CSW60 unaleta pamoja wawakilishi wa serikali na mashirika ya kiraia ambapo maudhui mwaka huu ni uwezeshaji wanawake na uhusiano wake katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.