Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya kisiasa ya UM kuanzishwa Colombia

Ofisi ya kisiasa ya UM kuanzishwa Colombia

Baraza la usalama la Umoja Mataifa leo limepitisha azimio la kuanzisha ofisi yake ya kisiasa nchini Colombia.

Azimio hilo pamoja na mambo mengine limezingatia ombi la serikali ya Colombia kwa Umoja wa Mataifa la kutaka uwepo wa ofisi hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa makubaliano ya kumaliza mzozo yanayotarajiwa kutiwa saini baina yake na kukundi cha FARC-EP.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuwa na kipengele cha upande wa tatu wa kusimamia na kuthibitisha utekelezaji wake ambapo ndio msingi wa kuanzishwa kwa ofisi hiyo itakayobeba jukumu hilo.

Ofisi hiyo itakayokuwa na jukumu la kuratibu itafanya kazi mwa muda wa mwaka mmoja ambapo Baraza limesema kuongezwa kwa muda kutategemea ombi la serikali na kikundi hicho cha FARC-EP.

Azimio hilo limesema ofisi itaongozwa na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na imemtaka Katibu Mkuuu awasilishe kwenye baraza mapendekezo ya utendaji na ukubwa wa ofisi hiyo, huku mwakilishi huyo akitakuwa kuwa anaripoti barazani shughuli za ofisi hiyo kila baada ya siku 90.