Skip to main content

MONUSCO bado kuamua kuhusu usaidizi wake kwa uchaguzi DRC

MONUSCO bado kuamua kuhusu usaidizi wake kwa uchaguzi DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO umeeleza utayari wake wa kusaidia tume ya kitaifa ya uchaguzi CENI katika maandalizi ya uchaguzi nchini humo lakini bado kiwango cha usaidizi chapaswa kuamuliwa.

Hii ni kwa mujibu wa video zilizotolewa na MONUSCO baada ya ziara ya rais wa CENI kwenye eneo la Kivu Kaskazini ili kutathmini hali ya maandalizi ya mchakato wa mapitio ya daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Rais wa CENI Corneille Nangaa Yobeluo amesema kwamba MONUSCO imekubali kutoa usaidizi wa usafiri katika utaratibu huo.

Kwa upande wake mkuu wa ofisi ya MONUSCO Kivu Kaskazini Daniel Ruiz amesema MONUSCO imetoa usadizi katika uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 na kwa mwaka huu

(Sauti ya bwana Ruiz)

“ Usaidizi kwa uchaguzi huo bado unapaswa kuzungumzwa kwenye makao makuu kufahamu kiwango chake. Kwa kweli taasisi za serikali zimebadilika sana tangu wakati ule, na tunapswa kuelewana kuhusu kiwango cha usaidizi wa pande zote.”