Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa hofu na mkwamo wa serikali ya mpito Sudan Kusini.

Ban atiwa hofu na mkwamo wa serikali ya mpito Sudan Kusini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon ameelezea hofu yake kuhusu mkwamo kwa pande zote Sudan Kusini dhidi ya kuanzisha majimbo 28 na kushindwa kwao kukamilisha miayadi ya tarehe 22 Januari ya kuanzisha serikali ya mpuito ya Umoja wa kitaifa nchini Sudan Kusini.

Amesisitiza kwamba kuundwa kwa serikali ya mpito ni hatua muhimu katika kutekeleza makubaliano ya Amani na kuweka msingi wa utulivu na Amani ya kudumu nchini humo. Stephane Dijarric ni msemaji wa Umoja wa mataifa

(SAUTI YA DUJARRIC)

"Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande husika kutupilia mbali tofauti zao. Amesihi mamlaka ya IGAD na Muungano wa AFrika kutumia fursa ya sasa ya mkutano ujao wa viongozi wa Muungano wa Afrika kushughulikia mkwamo wa kisiasa ambao unakwamisha kuanzishwa kwa serikali ya mpito ya Umoja wa kitaifa."

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon tarehe 28 mwezi huu ataelekea Addis Ababa Ethiopia kushiriki mkutano wa 26 wa viongozi wa Muungano wa Afrika.

Ban atahutubia mkutano huo tarehe 30, mkutano ambao maudhui yake ni mwaka 2016 na haki za binadamu ukijikita zaidi katika haki za wanawake, na atatumia uwepo wake Addis Ababa kuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali.