Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi dhidi ya magari ya vikosi vya Israel

Ban alaani mashambulizi dhidi ya magari ya vikosi vya Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani mashambulizi ya jana dhidi ya magari mawili ya vikosi vya julinzi vya Israel katika eneo la mashamba ya Sheba’a mashambulizi ambayo Hizbullah imedai kuhusika.

Katibu Mkuu ameelezea hofu yake dhidi ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya vikosi vya Israel kusini mwa Lebanon , eneo ambalo vikosi vya mpango wa Umoja wa mataifa nchini Lebanon UNIFIL vinaendesha operesheni zake.

UNIFIL na mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa Lebanon wamechukua hatua kwa kuwasiliana na pande zote kuhakikisha wanarejesha hali ya utulivu katika eneo hilo. UNIFIL pia inafanya uchunguzi wa tukio hilo kwa ushirika na jeshi la Lebanon na vikosi vya ulinzi vya Israel.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande zote kudumisha usitishwaji wa machafuko na kuhakikisha azimio la baraza la usalama nambari 1702 la mwaka 2006 linaheshimiwa.