Mwalikishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu Syria yuko ziarani Riyadh

Mwalikishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu Syria yuko ziarani Riyadh

Mwakilishi maalumu wa Katibu mKuu wa Umoja wa mataifa kuhusu Syria Bwana Staffan de Mistura yuko ziarani Riyadhi.

Katika ziara yake atatathimini athari za mvutano unaoendelea baiana ya Iran na Saudi Arabia  katika muafaka wa Vienna kuhusu mchakato wa kuleta Amani Syria.

Bwana De Mistura anaamini kwamba mtafaruku wa uhusiano baiana ya Iran na Saudia ni suala linalotia wasiwasi na amesisitiza haja ya kuhakikisha hali hiyo haitasababisha mlolongo wa athari katika ukanda mzima.

Baadaye wiki hii Bwana Demistura anatarajiwa kuzuru Iran.