Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inatathimini ripoti ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto CAR:

UNICEF inatathimini ripoti ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto CAR:

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa taarifa kufuatia ripoti ya uchunguzi huru kuhusu ukatili wa kingono dhidi ya watoto nchini Jamhuri ya afrika ya Kati CAR.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo UNICEf inatathimini ripoti hiyo na hasa inapotajwa kuwa ilishindwa kutekeleza sera zake za kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kingono na unyanyasaji wa watoto ili iweze kujufunza kwa siku za usoni.

UNICEF imesema inajutia hali hiyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kufuatilia maisha ya watoto. Imeongeza kuwa tayari imeanzisha mfumo mpya wa kutoa taarifa ndani ya UNICEF ili kuboresha usimamizi wa ndani wa mwitikio wa kuchukua hatua kwa ripoti za ukatili.