Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna ongezeko la wakimbizi wa ndani Burundi: Mbilinyi

Hakuna ongezeko la wakimbizi wa ndani Burundi: Mbilinyi

Wakati hali ya kiusalama ikizorota nchini Burundi hususani jijini Bujumbura, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini humo limesema licha ya hali mbaya ya kibinadamu, hakuna ripoti za ongezeko la wakimbizi wa ndani licha ya fununu za ongezeko hilo kwa wakimbizi wanaosaka hifadhi nje ya nchi.

Akizungumza na idhaa hii katika maojiano maalum, mwakilishi mkazi wa UNHCR, Burundi Abel Mbilinyi amesema hali imeanza kuimarika hivi sasa ikilinganishwa na mwishoni mwa juma na kuhuzu wakimbizi.

(SAUTI MBILINYI)

Amesema makamu wa Rais amewahakikishia wanadiplomasia katika kikao maaluma kuwa serikali imedhibiti vurugu hizo nakueleza kuwa UNHCR imejipanga kusaidia wakimbizi ikiwa kutakuwa na uhitaji.

(SAUTI MBILINYI)

Zaidi ya watu 80 wakiwamo maafisa usalama walifariki wakati wa machafuko mwishoni mwa juma.