Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO, Ulaya wajadili afya za wahamiaji

WHO, Ulaya wajadili afya za wahamiaji

Shirika la afya ulimwenguni WHO na wadau wa afya barani Ulaya wanakutana kujadili changamoto kuu, mahitaji na vipaumbele vya afya wanazokabiliana nazo wakimbizi na wahamiaji barani humo.

Mkutano huu unafanyika wakati huu ambapo wahamiaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanamiminika barani Ulaya kusaka hifadhi.

Taarifa ya WHO inasema kuwa mkutano huo unaofanyika nchini Italia umefunguliwa leo mjini Roma ambapo wahudhuriaji ni pamoja na mawaziri na  wawakilishi wa juu kutoka ukanda wa WHO barani Ulaya na maeneo mengine.

Washiriki watajadili jinsi gani nchi na mashirika yanavyoweza kuimarisha mifumo ya afya kwa wakimbizi na wahamiaji, lengo likiwa ni kuafikiana mbinu na mkakati mmoja kwa ajili ya utatuzi wa mahitaji ya afya kwa makundi hayo, imesema taarifa ya WHO