Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 20 tangu COP1 hali ya hewa imechochea zaidi majanga:Ripoti

Miaka 20 tangu COP1 hali ya hewa imechochea zaidi majanga:Ripoti

Ripoti mpya kuhusu majanga duniani imeonyesha kuwa asilimia 90 ya majanga yanahusiana na hali ya hewa huku Marekani, China, India, Ufilipino na Indonesia zikibeba mzigo wa nchi athirika zaidi. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Ikiwa imeangazia tathmini ya miaka 20, ripoti  hiyo iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga, UNISDR imetaja majanga hayo kuwa ni mafuriko, vimbunga, mawimbi joto, ukame na matukio mengine yatokanayo na hali ya hewa.

Tathmini  imeanzia mwaka 1995 ulipofanyika mkutano wa kwanza wa nchi wanachama wa makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi, COP1  ikionyesha kuwa  watu zaidi ya Laki Sita wamepoteza maisha, wengine zaidi ya Bilioni Moja wakijeruhiwa na kupoteza makazi yao.

Mkuu wa UNISDR Margareta Wahlström, anasema hali ya hewa ni vichochea vya hatari na hivyo mkutano wa COP21 una jukumu kubwa kwa kuwa...

(Sauti ya Wahlstrom)

 "Mwaka huu tumeshuhudia jinsi ambavyo majanga yameibuka katika nchi mbali mbali ikiwemo kimbunga  Patricia na Pam huko pasifiki, sasa Elnino kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka hamsini ikijumuishwa kwenye athari za mabadiliko ya tabianchi, moto wa vichakani na ukame kote ulimwenguni na sio tu katika nchi maskini bali pia katika nchi zenye uchumi wa juu zaidi ambako athari za ukame zinagharimu nchi."