Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasiwasi kuhusu hali ya hewa yasababisha bei za vyakula kupanda

Wasiwasi kuhusu hali ya hewa yasababisha bei za vyakula kupanda

Bei za vyakula zimeongezeka kwa asilimia 3.9 mwezi Oktoba ikilinganishwa na mwezi Septemba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Chakula na Kilimo FAO.

Hii ni mara ya kwanza baada ya bei za vyakula kupungua kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Hata hivyo bado kiwango cha bei za vyakula ni kidogo kikilinganishwa na mwaka uliopita.

Bei zilizopanda zaidi ni sukari, mafuta ya mawese na maziwa, FAO ikieleza kwamba ongezeko hilo limesababishwa na wasiwasi kuhusu mvua za El-Niño na hatari za ukame kwenye maeneo yanayozalisha bidhaa hizo.