Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi nchini Rwanda waeelezea matumaini yao

Wakimbizi wa Burundi nchini Rwanda waeelezea matumaini yao

Idadi ya wakimbizi wa Burundi waliotafuta hifadhi nchini Rwanda imefikia 68,000 mwezi Septemba mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini humo. Nusu yao ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.

Kwenye kambi ya Mahama iliyoko Mashariki mwa nchi, familia zinaendelea na maisha licha ya kuwa wengi wao wamepoteza mali zao na wamekataa tamaa.  Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii akisimulia masaibu na matumaini ya wakimbizi hao.