Raia wa Cote d’Ivoire pigeni kura: Ban

23 Oktoba 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaomba raia wa Cote d’Ivoire washiriki uchaguzi wa jumapili hii, tarehe 25, Oktoba.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa akikaribisha jitihada za wadau wote wa kisiasa za kushiriki utaratibu wa demokrasia kwa njia ya amani na uwazi.

Amesema kwamba msimamo huo utahakikisha matokeo ya uchaguzi ni chaguo la wananchi, akiongeza kwamba mafanikio ya utaratibu huo ni wajibu wa wadau wote.

Aidha Bwana Ban amekariri wito wake kwa viongozi wa kisiasa na wafuasi wao wa kuendelea kutatua sintofahamu zao kwa njia ya mazungumzo na amani, na kwa kuheshimu sheria ya katiba ya Cote d’Ivoire.

Hatimaye Katibu Mkuu amesisitiza msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia utaratibu wa uchaguzi nchini humo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter