Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen inamwaga damu: Ismail Ould Cheikh Ahmed

Yemen inamwaga damu: Ismail Ould Cheikh Ahmed

Taifa la Yemen liko katika sintofahamu huku vita ya wenyewe kwa wenyewe ikiendelea, amesema mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Ismail Ould Cheikh Ahmed wakati akilihutubia baraza la usalama hii leo.

Bwana Ahmed amelieleza baraza hilo hali tete ya taifa hilo ambalo limeshuhudia machafuko kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na mgogoro wa vikosi vya serikali na waasi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2000.

"Yemen inawaka moto na watu wake wako katika sintofahamu. Nchi inamwaga damu huku miji ikiharibika. Raia wanapokonywa haki za msingi."

Majadiliano ya kisiasa kati ya serikali na waasi wa Houthi yamepoteza matumaini kufuatia muundo mpya wa masharti .

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ameshauri majadiliano mapya na sasa anazungumza na pande kinzani ili kukubaliana ajenda, tarehe na muundo wa mikutano.

Wakati huo huo wanachama wa baraza la uslama la Umoja wa Mataifa wamekaribishsha tangazo la mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UM kuhusu mazungumzo tarajiwa. Wamepongeza umauzi wa serikali ya Yemen wa kushiriki mazungumzo ya amani na wadau wengine.