Kikosi cha pamoja cha Afrika cha ulinzi wa amani kuzinduliwa:Brigedia Ahmed

Kikosi cha pamoja cha Afrika cha ulinzi wa amani kuzinduliwa:Brigedia Ahmed

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Umoja wa Mataifa, suala la ulinzi wa amani bado linasalia kuwa mojawapo ya jukumu muhimu la Umoja huo ambapo mataifa ya Afrika yamekuwa mstari wa mbele  kuchangia  wanajeshi na askari polisi katika operesheni za ulinzi wa amani za umoja huo.

Katika mahojiano na Idhaa hii kuhusu hatma ya operesheni hizo, Brigedia Jenerali  Ahmed Mohamed ambaye ni mnadhimu mkuu wa ofisi ya kijeshi ya Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa amesema hatua zimechukuliwa kuimarisha ushiriki wa Afrika kwenye operesheni hizo kwa kuunda kikosi cha pamoja kinachokuwa tayari wakati wowote, ASF.

(SAUTI Ahmed)

Kikosi hicho, ASF kinalenga kuwezesha nchi za Afrika kupeleka mara moja askari pindi mzozo unapotokea katika nchi wanachama badala ya kusubiri mchango wa nchi moja moja.