Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saratani ni changamoto kubwa Tanzania asema manusura wa saratani ya titi Gloria Kida

Saratani ni changamoto kubwa Tanzania asema manusura wa saratani ya titi Gloria Kida

Nchini Marekani, asilimia 89 ya wagonjwa wa saratani ya titi wanaweza kupona, lakini ni chini ya asilimia 50 kwenye nchi zinazoendelea.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA, ambalo linaeleza kuwa tofauti hiyo imesababishwa na uhaba wa ujuzi na upatikanaji wa matibabu kwenye nchi hizo, ikiwemo Tanzania.

Gloria Kida ni manusura wa saratani ya matiti ambaye ameshiriki katika mkutano wa kimataifa kuhusu upatikanaji wa matibabu ya saratani kwenye nchi zenye kipato cha kati na cha chini uliofanyika hivi karibuni mjini Vienna, Austria, wakati wa kongamano la kila mwaka la IAEA.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte wa idhaa hii, akaeleza  kwamba IAEA imeunda mkakati uitwao PACT wenye lengo la kupunguza kwa theluthi moja idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa saratani kwa kipindi cha miaka kumi na tano ijayo katika nchi zinazoendelea, kupitia uhamasishaji wa jamii na upatikanaji wa vifaa vya vipimo na matibabu.

Hapo akaanza kwa kumweleza Priscilla hali ikoje nchini Tanzania.