Furaha yangu ni kuona watu wakipona upofu : Mshindi wa tuzo ya Mandela

Furaha yangu ni kuona watu wakipona upofu : Mshindi wa tuzo ya Mandela

Siku ya Umoja wa Mataifa ikiadhimishwa hapa katika Umoja wa Mataifa miongoni mwa matuko ni utolewaji wa kwanza wa tuzo za Nelson Rolihlahla Mandela ambapo miongoni mwa waliopokea tuzo hizo ni Dk Hellen Ndome kutoka Namibia ambaye ni dakatri wa macho.

Bi Ndome ambaye ameleta mabadiliko makubwa kwa kusaidia jamii ya Namibia kuweza kukabiliana na upofu kwa operesheni za kitaalamu amesema kazi hiyo aliyoifanya imekuwa ya kujitolea kwa moyo wa kusaidia lakini hujawa na furaha kubwa akiona wenye upofu wameweza kuona na kurejelea maisha ya kawadia.

Katika mahojinao maaluma na redio ya Umoaj wa Mataifa kabla ya kupokea tuzo Dk Ndome ameelezea mkasa wa mama aliyepata upofu na kutibiwa kisha kupona akisema

(SAUTI DK NDOME)

‘‘Ajuza huyu mwanamke alikwua na watoto watatu, na wote walikufa kwa HIV, alisalia na wajuku na alikuwa haoni. Furaha aliyokuw ana yo baada ya kuona tena ilikuwa ya jabu. Aliweza kwenda kuwaangalia wajukuuu wake. ‘’

Pamoja na Dk Ndome, Rais mstaafu wa Ureno wa Jorge Sampaio naye amepewa tuzo kwa mchango wake katika taifa hilo.