Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya zazorota Somalia: WHO

Huduma za afya zazorota Somalia: WHO

Kuna hofu ya kuzorota kwa huduma za afya nchini Somalia wakati ambapo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema jamii ya Kimataifa imeelekeza ufadhili mkubwa kwa mchakato wa kisiasa na usalama katika nchi hiyo iliyozongwa na mapigano. Taarifa kamili na John Kibego(Taarifa ya John Kibego)

Wadau wa afya nchini humo wanatabiri kupungua zaidi katika utoaji wa huduma za kuokoa maisha kutokana na ukosefu wa ufadhili wa kibinadamu kulingana na makadirio ya ufadhili wa mwaka 2015 na 2016.

Tayari katika miezi mitau iliyopita, angalau hospitali 10 aidha zimefungwa ama kuathiriwa vibaya na pengo la ufadhili wakati ambapo mashirika mengi yakiwemo Save the Children na Ofisi ya Umojwa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA) yanatarajiwa kusitisha misaada kwa hospitali mbali mbali nchini mnamo mwaka huu.

Kwa sasa kuna Wasomali milioni 3.2 wanaohitaji msaada wa kibinadamu, huku  sekta ya afya ikiwa na ufadhili wa asilimia 8.5,  kiwango cha chini zaidi tangu mwaka 2008.