Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufaransa yaombwa kupeleka mbele ya sheria wanajeshi walioshatakiwa kubaka

Ufaransa yaombwa kupeleka mbele ya sheria wanajeshi walioshatakiwa kubaka

Kamati ya Haki za binadamu leo imesema imeisihi Ufaransa kupeleka mbele ya sheria wanajeshi wanaowajibika katika kesi ya uhalifu wa kijinsia dhidi ya watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Wito huo umetolewa leo mjini Geneva, kamati ya haki za binadamu ikikutana kujadili hali iliyopo nchini Ufaransa, pamoja na nchi sita nyingine, ikiwemo Uingereza na Canada.

Baadhi ya wanajeshi wa Ufaransa wanadaiwa kuwa wamejihusisha na vitendo vya ubakaji na uhalifu wa kijinsia dhidi ya watoto wakati wa operesheni zao za kulinda amani nchini CAR kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014, kabla jukumu hilo halijapewa kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Akijibu maombi hayo,mwakilishi  wa Ufaransa umesema kwamba uchunguzi unaendelea.

Fabian Salvioli ni mwenyekiti wa kamati ya Haki za binadamu.

(SAUTI FABIAN)

Wameanza uchunguzi na uwakilishi wa Ufaransa umesema kwa kweli ni jambo muhimu, na tumeanza mashtaka, lakini hatuna taarifa zaidi.”