Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi Yemen yaitia wasiwasi ofisi ya haki za binadamu

Mashambulizi Yemen yaitia wasiwasi ofisi ya haki za binadamu

Mashambulizi yanayoendelea nchini Yemen ni tishio dhidi ya haki za raia wa kawaida, imesema leo ofisi ya haki za binadamu, huku idadi ya wahanga ikizidi kuongezeka, na hali ya kibinadamu kuzorota zaidi. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Rupert Colville, amesema mashambulizi kutoka kwa pande zote za mzozo yameripotiwa dhidi ya maeneo ya makazi, pia miskiti na masoko, yakilenga raia moja kwa moja kwa kutumia risasi, mabomu au makombora.

“Tunazikumbusha pande zote za mzozo kuwa shambulio lolote linalolenga raia moja kwa moja ni  ukiukaji mkubwa wa haki ya kimataifa ya kibinadamu. Masharti kuhusu kutofautisha malengo, kutumia umakini na uiano yanapaswa kuheshimiwa kabisa.”

Tangu mwanzoni mwa mapigano tarehe 26 Machi, watu 1,693 wameuawa na wengine 3,829 wamejeruhiwa.