Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lashauriana kuhusu mchango wa teknohama

Baraza Kuu lashauriana kuhusu mchango wa teknohama

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya mashauriano kuhusu kongamano la dunia kuhusu habari, WSIS, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tathmini ya ngazi ya juu ya Baraza hilo kuhusu utetekelezaji wa makubaliano ya awali ya kongamano la WSIS.

Akizungumza wakati wa mkutano wa leo, rais wa Baraza Kuu, Sam Kutesa, amesema kuwa WSIS ilikuwa ni hatua muhimu katika juhudi za kimataifa za kuimarisha nguvu za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) katika kuwezesha maendeleo.

Amesema kuongezeka kwa upatikanaji wa teknohama na huduma husika kumetoa fursa kubwa zaidi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo mengi ya dunia, akiongeza

Tathmini ya WSIS inafanyika wakati ambapo jamii ya kimataifa inajishughulisha na kubuni ajenda ya mabadiliko ya maendeleo baada yam waka 2015. Ni muhimu kwamba, kupitia tathmini hii, sio tu tupime hatua zilizopigwa, bali pia kuongeza kasi kufungua uwezo wa technolojia ya habari na mawasiliano kuchangia utimizaji wa madeneleo endelevu.”

Licha ya hayo, Kutesa amesema bado kuna changamoto, zikiwemo za kupunguza pengo la walio kwenye mitandao ya kidijitali na wasio weza kuifikia, na katika kutumia teknohama kuchochea maendeleo jumuishi.