Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi huru hauwezi kufanyika Burundi kwa hali ilivyo sasa : mtalaam wa UN

Uchaguzi huru hauwezi kufanyika Burundi kwa hali ilivyo sasa : mtalaam wa UN

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukuzaji wa ukweli, haki, ulipaji fidia na sheria wakati wa mpito, Pablo de Greiff amesema uchaguzi huru hauwezi kufanyika nchini Burundi kwa sababu ya mazingira yaliyopo sasa hivi ya ukatili, mateso na vitisho.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, mtalaam huyo ameeleza kwamba makubaliano ya Arusha ya 2000 na katiba ya 2005 viliweza kuleta mabadiliko makubwa nchini humo, kwa kuwezesha kugawana madaraka na kupunguza mvutano wa kikabila.

Licha ya hayo mwelekeo wa kampeni ya uchaguzi huu unahatarisha mshikamano huo, amesema mtalaam wa Umoja wa Mataifa, akieleeleza wasiwasi wake kuhusu hatari za kurejea kwa mzozo wa kikabila.

Aidha bwana de Greiff amesema ni wajibu wa jamii ya kimataifa kuongeza ufuatiliaji wa uhalifu unaofanyika nchini humo.

Hatimaye amesema ni muhimu kukabiliana na sababu za msingi zilizochochea vurugu nchini humo, kwa kupambana na utamaduni wa ukwepaji sheria, kusaida wahanga wa vitendo vya uhalifu uliofanyika zamani na kumulika ukweli kuhusu uhalifu huo, na kuleta mabadiliko katika sekta ya sheria, usalama na elimu.