Skip to main content

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2015

Mtihani wa kujiunga na UM kwa vijana waliobobea kitaaluma, 2015

Kila mwaka, Umoja wa Mataifa hutafuta vijana waliobobea katika fani mbali mbali, ambao wapo tayari kuanza huduma ya kitaaluma kama wahudumu wa kimataifa wa umma. Mpango wa Vijana Waliobobea Kitaaluma, yaani YPP, huleta vipaji vipya kwa Umoja wa Mataifa kupitia kwa mtihani wa kila mwaka.

Mwaka huu wa 2015, mtihani utafanyika mnamo tarehe 4 Disemba katika fani za Usimamizi, Masuala ya fedha, Mifumo ya takwimu, habari, masuala ya kijamii na Masuala ya Sheria.

Ili kushiriki mtihani huu, ni lazima uwe unatoka nchi zilizoorodheshwa kushiriki mwaka 2014, uwe na shahada ya kwanza, uwe unaongea Kiingereza au Kifaransa sanifu, na uwe na umri wa miaka 32 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Utatakiwa kufanya ombi la kushiriki mtihani huu kati ya tarehe zifuatazo

Mei 20 hadi Julai 19 -     Usimamizi

Mei 27 hadi Julai 26 -      Fedha

Juni 03 hadi Agosti 02 - Takwimu

Juni 10 hadi Agosti 09 - Habari

Juni 17 hadi Agosti 16– Masuala ya Kijamii

Juni 24 hadi Agosti 23– Masuala ya Sheria

Kumbuka, itakuwa vyema ikiwa utakamilisha na kuwasilisha maelezo yote kwa njia sahihi na nadhifu kwani hicho kitakuwa kigezo cha kupima uwezo wa wako kukubaliwa kuufanya mtihani.

Kumbuka pia kuwa, maombi ambayo hayatakamilishwa vyema au yatakayochelewa kuwasilishwa hayatakubaliwa, kwa hiyo ni lazima uwasilishe ombi lako kabla ya tarehe ya ukomo.

Kuona kama nchi yako inashiriki,  na maelezo zaidi, tembelea tovuti:

http://bit.ly/1aAemgZ

Mtihani

Mtihani umegawika katika sehemu mbili: sehemu ya kwanza ambayo ni kwa kuandika, itatahini upana wa ujuzi wako, uwezo wa kutathmini mambo, na uwezo wa kuandika nakala muhimu.

Sehemu ya pili ni kwa wale wanaopita ule wa kwanza pakee, na ni aina ya mahojiano