Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujerumani yaupiga jeki mfuko wa kibinadamu wa Sudan kwa dola 1,000,000

Ujerumani yaupiga jeki mfuko wa kibinadamu wa Sudan kwa dola 1,000,000

Serikali ya Ujerumani imetoa mchango wa Euro milioni moja, sawa na dola milioni moja, kwa mfuko wa pamoja wa kibinadamu kwa Sudan mwaka 2015.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kuuchangia mfuko huo, ingawa imekuwa msaidizi wa kutegemewa kwa Sudan tangu mwaka 2000.

Balozi wa Ujerumani Sudan, Rolf Welberts, amesema kwa kuwa kuna watu wengi walio hatarini maeneo mengi Sudan, usaidizi kwa wakati na usio wa ukiritimba ni muhimu sana.

Naye Mratibu wa masuala ya kibinadamu Sudan, El-Mostafa Benlamlih, amesema kuwa ufadhili wa kibinadamu Sudan umekuwa haba kwa sababu wafadhili wameelekeza juhudi zao kwa mizozo mingineyo ya kikanda.