Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa wito waongezeke wanaojitolea kutoa damu kuokoa maisha

WHO yatoa wito waongezeke wanaojitolea kutoa damu kuokoa maisha

Wakati Siku ya utoaji damu duniani ikikribia kuadhimishwa mnamo Juni 14, Shirika la Afya Duniani, WHO limetoa wito uongezeke utoaji damu wa kujitolea ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani kila mwaka.

Kauli mbiu ya kampeni ya mwaka huu ni, “Ahsante kwa kunusuru uhai wangu”, ikitoa msukumo kwa watoaji damu wa kujitolea kutoa damu kutoa damu mara kwa mara, kwa ujumbe, “Toa bure, toa mara kwa mara. Utoaji damu ni muhimu.”

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Margaret Chan amesema njia bora ya kuhakikisha kuna upatikanaji wa damu salama naya kutosha, ni kuwa na utoaji wa damu mara kwa mara wa wale wanaojitolea, bila malipo. Amesema WHO inazihimiza nchi wanachama kupata damu inayohitajika kutoka kwa watu wa kujitolea.