Skip to main content

Ban atiwa hofu na ongezeko la mashambulizi dhidi ya walinda Amani wa UNAMID

Ban atiwa hofu na ongezeko la mashambulizi dhidi ya walinda Amani wa UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa hofu na ongezeko la karibuni la mashambulizi dhidi ya walinda Amani wa mpango wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Dafur Sudan, na ushirikiano mdogo unaotolewa na serikali ya Sudan kushughulikia matukio hayo.

Katibu Mkuu amelaani mashambulio mawili yaliyofanywa na kundi la watu wasijulikana wenye silaha kwenye eneo la Kass Dafur Kusini April 23 na 24 ambapo walinda Amani sita wa UNAMID walijeruhiwa na washambuliaji wane waliuawa , walinda Amani walipojibu mapigo kwa kujihami.

Ban ameitaka serikali ya Sudan kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa kwenye mkono wa sharia na kuchukua hatua zote za lazima kuepuka mashambulizi au vitisho Zaidi dhidi ya walinda Amani jimboni Darfur.

UNAMID imeanzisha uchunguzi wake kufuatia mashambulizi hayo. Ban pia amesema amesikitishwa na kitendo cha tarehe 26 April cha serikali kukataa ombi la kumhamisha kwa dharura kwa ajili ya matibabu mlinda Amani wa Ethiopia aliyejeruhiwa akiwa kazini mjini Kujkar Magharibi mwa Dafur.