Skip to main content

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Liberia

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Liberia

Baraza la Usalama leo limepitisha azimio la kupunguza kwa asilimia 25 idadi ya walinda amani kwenye Ujumbe wa Umojawa Mataifa nchini Liberia, UNMIL. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Uamuzi wa Baraza la Usalama ni hatua ya tatu katika kutekeleza mpango wa kuondoa UNMIL Liberia. Utekelezaji wa mpango huo ulikuwa umesitishwa tangu Septemba mwaka 2014 kutokana na hatari zilizotokana na mlipuko wa Ebola.

Kwa muijbu wa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous aliyezungumzia hali iliyopo nchini Liberia kwenye Baraza la Usalama, tarehe 16 Machi, hali ya usalama na utulivu imerejea Liberia, mlipuko wa Ebola ukikaribia kudhibitiwa. Na kwa hiyo, wanachama wa baraza la Usalama wameamua kupunguza idadi ya walinda amani na nguvu za polisi za UNMIL.

Aidha azimio limeelezea wasiwasi wa wanachama wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya usalama kwenye mpaka wa Liberia na Côte d’Ivoire, likiziomba serikali za nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano wao katika swala hilo.

Hatimaye, azimio linakariri matarajio ya Baraza la Usalama ya kuona ukomo wa mamlaka ya UNMIL ifikapo Juni, mwaka 2016.