Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yazindua mwongozo wa kuimarisha utawala wa sheria Somaliland

UNODC yazindua mwongozo wa kuimarisha utawala wa sheria Somaliland

Mwongozo mpya wa kuimarisha mfumo wa sheria wa jimbo la Somaliland, Somalia umezinduliwa na Shirika la inayohusika na madawa na uhalifu katika Umoja wa Mataifa, UNODC.

Chombo hicho ambacho kimeundwa ili kitumiwe na polisi, waendesha mashtaka, wanasheria na majaji katika jimbo hilo, kinatoa mwongozo wa kina kuhusu kuzuia uhalifu na sheria ya uhalifu.

Dhamira kuu ya chombo hicho ni kuboresha taasisi za sheria na kuimarisha mfumo rasmi wa sheria wa jimbo la Somaliland.

Ingawa kesi nyingi za uhalifu katika jimbo la Somaliland hutatuliwa kupitia mifumo ya sheria ya kijadi au Sharia’h, kutumia mfumo rasmi unaouiana vyema na viwango vya kimataifa huenda ukawa ndio mfumo mbadala unaofaa zaidi.