Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na viongozi wa Japan kando ya mkutano wa kupunguza majanga

Ban akutana na viongozi wa Japan kando ya mkutano wa kupunguza majanga

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na viongozi wa serikali ya Japan kandoni mwa mkutano wa kupunguza majanga unaoendelea mjini Sendai.

Miongoni mwa viongozi hao ni Bwana Natsuo Yamaguchi, mbunge na mwakilishi mkuu wa chama cha  Komeito , na pia bwana Nobutaka Machimura, spika wa bunge la Japan.Katika mkutano wao Ban ameipongeza Japan kwa msaada mkubwa katika kazi za Umoja wa Mataifa.

Pia viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ajenda za Umoja wa Mataifa ikiwemo shughuli za kulinda amani, maendeleo, misaada ya kibinadamu, ulinzi wa binadamu na kuwawezesha wanawake.

Katibu Mkuu mbali ya kushukuru juhudi za serikali amesisitiza jukumu kubwa na muhimu la bunge katika ushawishi wa kupata fedha na msaada wmingine kwa ajenda za Umoja wa Mataifa.