Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ya Marekani kutofungia mitandao ya internet ni ushindi kwa uhuru wa kujieleza

Hatua ya Marekani kutofungia mitandao ya internet ni ushindi kwa uhuru wa kujieleza

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na wa kujieleza  David Kaye, leo amekaribisha hatua ya tume ya mawasiliano ya Marekani FCC kuanzisha kanuni mpya za kulinda  uhuru katika mtandao wa intaneti nchini humu.

Sheria za FCC zitasaidia uhuru na uwazi wa mtandao wa intaneti na kuhakikisha watu wanaweza kuendelea kupata kwa kila kitu kisichovunja sheria kwenye mtandao bila vikwazo au kuingiliwa kwa watoa huduma za mtandao wa intaneti.

Marekani inafuata mataifa mengine  kama vile Brazil, Chile na Uholanzi ambayo tayari yamepitisha sheria kama hizo kuhusu mtandao wa intaneti.

Bwana Kaye amesema huu ni ushindi mkubwa kwa uhuru wa kujieleza na fursa ya kupata habari nchini Marekani, akiongeza kuwa anatumai sheria hizo mpya zitakuwa ni mfano wa kuigwa na serikali za nchi zingine ili kulinda au kupanua wigo wazi na huru wa intaneti.