Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu na utumikishwaji wa watu ukomeshwe: Balozi Brown

Usafirishaji haramu na utumikishwaji wa watu ukomeshwe: Balozi Brown

Ni aibu kujadili usafirishaji haramu wa binadamu na utumikishwaji katika karne ya 21, wamesema wawakilishi wa nchi na taasisi mbalimbali wakati wa mkutano kuhusu  ukomeshwaji wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na haki za bindamu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Akizungumza katika mkutano huo mwakilishi wa kudumu wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa Harold Brown anataja sababua za aina mpya ya utumikishwaji wa binadamu na kutaka ukomeshwahji haraka

(SAUTI HAROLD)

"Ni umasikini na umaskini uliokithiri na mengineyo yanayosababisha aina mpya ya utumikishwaji na aina nyingine za utumwa. Wafanyakazi wahamaijai na watu asilia wako katika mazingira hatarishi ya kutumikishwa."

Takribani watu milioni 20 kote duniani ni wahanga wa utumikishwaji au usafirishaji haramu wa binadamu.