Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aridhia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi wa uchaguzi Burundi

Ban aridhia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi wa uchaguzi Burundi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameridhia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi wa uchaguzi nchini Burundi, MENUB kuanza kazi zake rasmi tarehe moja January 2015 kwa mujibu wa mamlaka ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika taarifa kutoka kwa ofisi ya Msemaji wa Katibu Mkuu, ujumbe wa MENUB utaongozwa na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu, Cassam Uteem kutoka Mauritius, na ujumbe huo utafuatilia na kuripoti juu ya uchaguzi wa urais, wabunge na serikali za mitaa uliopangwa kufanyika kati ya Mei na Septemba 2015.
Aidha, Katibu Mkuu amema kuwa uchaguzi wa amani na kuaminika ni muhimu kwa watu wa Burundi, na anatumai kwamba wananchi wa Burundi wote watachukua fursa hiyo kuimarisha amani na utulivu katika nchi yao.