Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uamuzi wa msichana anayeishi na virusi vya HIV unatia moyo:Kenya

Picha ya UNAIDS

Uamuzi wa msichana anayeishi na virusi vya HIV unatia moyo:Kenya

Wakati ukomo wa malengo ya maendeleo ya Milenia ikiwemo lile namba sita la kutokomeza HIV/AIDS, Malaria na magonjwa mengine ukielekea ukingoni,  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya ugonjwa huo,UNAIDS limetaka hatua zaidi zichukuliwe ili kuhakikisha Ukimwi unakuwa umetokomezwa ifikapo mwaka 2030

. Moja ya hatua ilizozitaja ni umuhimu wa mtu kupima afya yake na kufahamu hali yake, hatua ambayo inamwezesha hata anayebainika kuwa na virusi hivyo kuishi maisha chanya na kuepusha maambukizi zaidi.

Katika makala ifuatayo Salim Chiro wa Radio washirika Pwani fm iliko nchini Kenya amekutana na msichana ambaye amepima afya na kutambua kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi na hatua alizochukua na sasa anaishi maisha mazuri ungana naye.