Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya Haki za Binadamu yataka nchi kutokomeza adhabu ya kifo

Umoja wa Mataifa @UM

Kamati ya Haki za Binadamu yataka nchi kutokomeza adhabu ya kifo

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imeyataka mataifa duniani kuridhia itifaki ya kimataifa ambayo inataka ukomeshwaji wa adhabu ya kifo.

Itifaki hiyo ya awamu ya pili inayoangazia haki za kiraia na kisiasa inatoa mwongozo kwa mataifa wanachama kuondokana na adhabu ya kifo adhabu ambayo bado inatekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani.

Tangu kuasisi kwake itifaki hiyo ni mataifa machache tu yaliyoridhia hali iliyofanya juhudi za kukabiliana na adhabu ya kifo duniani kukosa mafanikio yaliyotarajiwa.

Kamati hiyo imeyataka mataifa ambayo bado yanaendelea kutekeleza adhabu ya kifo kuchukua hatua za kuridhia itifaki hiyo ambayo inatumika kama chombo cha kuweza kukabiliana na adhabu hiyo.