Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo huru la uchunguzi Gaza lapata mjumbe mwingine

Umoja wa Mataifa

Jopo huru la uchunguzi Gaza lapata mjumbe mwingine

Hatimaye jopo lililoundwa kuchunguza operesheni za kijeshi zilizofanywa kwenye Ukanda wa Gaza limepata mjumbe wa tatu ambaye ni Jaji Mary McGowan Davis.

Rais wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Balozi Baudelaire Ndong Ella kutoka Gabon ametangaza uteuzi huo baada ya mjumbe wa awali Amal Alamuddin kusema hatoweza kushiriki kutokana na majukumu aliyo nayo.

Jaji Mary ataungana na Doudou Diène na William Schabas ambaye ni mwenyekiti na ambao uteuzi wao ulitangazwa tarehe 11 mwezi huu.

Tume hiyo huru iliyoundwa na barazahilokwa azimio namba S-21/1, inatarajiwa kubainisha ukiukwaji wowote wa sheria za kimataifa wakati wa operesheni ya kijeshi ya Israeil ya tarehe Nane Julai iliyopatiwa jina la Operation Protective Edge. Halikadhalika itabainisha watekelezaji na kupendekeza hatua za uwajibikaji.

Inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kweney kikao cha 28 cha Baraza la haki za binadamu mwezi Machi mwaka 2015.