Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay alaani vikali uhalifu unaofanywa na ISIL Iraq

UN Photo/Violaine Martin
Navi Pillay.

Pillay alaani vikali uhalifu unaofanywa na ISIL Iraq

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani vikali mauaji yanayoendelea kufanywa na waasi wa ISIL nchiniIraqambao wanadaiwa kuwalenga makundi ya watu kwa shabaha ya kuanzisha dola ya Kiislamu.

Waasi hao ambao wamekuwa wakiendesha vitendo viovu katika maeneo ya raia hivi sasa wanaripotiwa kuzidisha mauaji na wakiwalenga zaidi jamii za watu wachache wakiwemo wakristo, wayazidi na Turkomen.

Kutokana na hali hiyo Pillay amelionya kundihilona amelikumbusha namna linavyowajibika kuheshimu na kulinda haki za binadamu kwani vitendo vyao vinakwenda na sheria za kimataifa.

Ravina Shamdasani ni msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa MataifaGeneva.

(Sauti ya Ravina)

"Vitendo vya kutisha na kusikitisha vyenye kukiuka haki za binadamu vinatendwa kila siku na ISIL na makundi washirika kama hayo. Kamishna  wa haki za binadamu anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kuwa wahusika wa vitendo hivi vya kikatili hawakwepi mkono wa sheria. Mtu yeyote anayefanya, au kusaidia katika utekelezaji wa uhalifu wa kimataifa anapaswa kuwajibishwa "