Ban akutana na rais wa China

16 Agosti 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye amewasili leo China kwa ajili ya uzinduzi wa michezo ya Olimpiki ya vijana ya pili huko Nanjing, amekuwa na mazungumzo na rais wa China Xi Jinping.

Ban ametoa shukrani zake kwa jinsi China inavyounga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa za kuendeleza amani na usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu.

Katibu Mkuu na Rais wa China wamejadili masuala kadhaa ya kimataifa, yakiwemo hali ya Ukraine,, Iraq, Syria, Mashariki ya Kati, Gaza, Kaskazini mwa Asia na Korea. Wamezungumzia pia mlipuko wa Ebola.

Katibu Mkuu amepogeza pia China kwa dhima yake katika kupambana na changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi na ajenda ya mandeleo ya baada ya 2015.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud