Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo vya Ebola yaongezeka

Mhudumu wa afya akivalia sare ya kujikinga wakati wa kuwahudumia waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola,Kailahun,Sierra Leone.Picha:IRIN/Tommy Trenchard

Idadi ya vifo vya Ebola yaongezeka

Wakati mkutano wa dharura ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani, WHO unaendelea ili kutathmini iwapo mlipuko huo unaibua hofu ya kimataifa katika afya ya umma, idadi ya vifo vya Ebola imezidi kuongezeka, kwa mujibu wa WHO. Tayari watu 932 wameshafariki dunia kutoka nchi za Sierra Leone, Liberia, Guinea na hivi karibuni, Nigeria.

Fadela Chaib, msemaji wa WHO, amesema hatari ya kimataifa ikitambuliwa, WHO itatangaza shauri kuhusu hatua za kuchukua ili kuzuia maambukizi mengine kwa ngazi ya kimataifa, bila kukwamisha mno shughuli za usafiri na biashara.

“Mfululizo wa maambukizi ya Ebola haujasitishwa popote. Visa vingine vinaibuka kila siku, na tusipojituma na kuchangia nguvu zetu zote, kwa upande wa vifaa, utalaam na ufadhili, ili kusaidia Afrika ya Magharibi kupambana na ugonjwa huo ambao haukujulikana awali, itakuwa vigumu sana kwa nchi hizo, uchumi wao na raia wao, kupambana pekee yao na kitu kama Ebola

WHO imashazindua wito kwa ufadhili wa dola milioni 100 ili kupambana ma mlipuko huo wa Ebola, na kuzindua kituo cha mkoa cha kuratibu operesheni katika nchi zote zilizoathirika na ugonjwa huo.